panda1

Kategoria : Nomino
Ngeli : [i-/zi-]
  1. mahali ambapo njia imegawika na kuwa mbili au zaidi ; njia panda mahali barabara zinapokutana

panda2

Kategoria : Nomino
Ngeli : [i-/zi-]
  1. kijiti chenye sehemu mbili na kufungwa mpira wa kutupia jiwe dogo
Kisawe
  1. manati

panda3

Kategoria : Nomino
Ngeli : [i-/zi-]
  1. sehemu ya uso ambayo iko juu ya macho

panda4

Kategoria : Nomino
Ngeli : [i-/zi-]
  1. pembe kubwa yenye tundu nchani na hupigwa ili kutoa ujumbe au kutumbuiza
Kisawe
  1. baragumu

panda5

Kategoria : Nomino
Ngeli : [i-/zi-]
  1. tazama paji