Word of the Day
Learn Swahili everyday
Subscribe to receive KamusiOnline Word of the Day in your inbox
mweni
Kategoria : Nomino
Ngeli : [a-/wa-]
- mtu asiye mwenyeji wa mahali fulani
- mgeni
parokia
Kategoria : Nomino
Ngeli : [i-/zi-]
Entimologia : Kiingereza
- eneo ambalo lina kanisa lake na huhudumiwa na kasisi, hasa kwa waumini wa kikristo
- parishi
sitish.a
Kategoria : Kitenzi
- zuia jambo lisiendelee kufanyika; simamisha
' Wapiganaji walisitisha vita kwa muda.'
Mnyambuliko : sitishia, sitishika, sitishwa
wenzo
Kategoria : Nomino
Ngeli : [u-/zi-]
- chuma au kijiti kikubwa kinachotumiwa kuinulia au kukisogeza kitu kingine kwa mfano gogo, mwamba na kadhalika
- kitu kinachofanya kazi iwe rahisi
- Mti hauendi ila kwa nyenzo zake.
tumbawe
Kategoria : Nomino
Ngeli : [li-/ya-]
- jiwe jororo la baharini linalotokana na mkusanyiko wa vinyama vidogo vya baharini
- fufuwele
- bawe
- chawe